Tia Saini Azimio La Bogota Kuhusu #Hakizaushuru kwa #Hakizawanawake

Published on 
12/05/2017

Shirika lako limekaribishwa kutia saini ili kuunga mkono Azimio katika linki hii 

* Pata Azimio hili katika linki zifuatazo.

Kutoka Kusini hadi Kaskazini wanawake wametengwa kutoka kwa miundo na mifumo yenye nguvu inayotawala sera za uchumi wa kitaifa na wa kimataifa na miundo ya kifedha. Jamii zinazotetea haki za wanawake na haki za ushuru zinakubaliana na mtazamo huu. Jijini Bogota, nchini Colombia, mapema mwaka huu, watafiti, mawakili, watoa huduma za umma, wanachama wa vyama vya wafanyakazi, na wanaharakati kutoka kwa mavuguvugu ya haki za ushuru na haki za wanawake walikutana katika kikao cha kimataifa kilichojumuisha mashirika na wataalamu walio katika mstari wa mbele kwenye masuala haya. Lengo kuu lilikuwa ni kuunda na kuthibitisha misimamo imara na ya pamoja ambayo itatilia mkazo hatua za pamoja katika miaka ijayo: kuanzisha alama ya mabadiliko, kuanzia kwa hatua bainifu iliyo tofauti na imani za awali.

Azimio la Bogota kuhusu Haki za Ushuru kwa Haki za Wanawake, lililozaliwa kutokana na kikao hiki jijini Bogota, linafafanua maadili yaliyoafikiwa, na kudai haki za wanawake ambazo zinaweza kupatikana kwa mabadiliko ya kimuundo, kimfumo, kiutamaduni na kisera za kiuchumi. Mashirika tofauti yanakaribishwa kusambaza na kumiliki maono haya, kutia saini na kukubali kujitolea kwa Azimio na kufanya kazi na sisi  ili kufanikisha haki zote tofauti na anuwai za kimsingi  kwa wanawake.

Mashirika yanakaribishwa kutia saini na kuunga mkono Azimio hili katika linki hii

Pata Azimio hili kwa lugha mbali mbali (PDFs): 

                              in English                                                      بالعربية

                             en español                                                    en français

  

                             kwa Kiswahili                                               em português

Kampeni ya #Hakizaushuru kwa Haki za wanawake

Azimio la Bogota ni stakabadhi iliyotokana na kazi inayoendelea kuhusu kampeni za haki za ushuru kwa haki za wanawake. Tangu tarehe 8-24 Mechi mwaka huu, mamia ya mashirika kutoka kote ulimwenguni waliungana pamoja kwa harakati za kwanza za #HakiZaUshuru kwa Siku za Hatua za Haki za Wanawake Ulimwenguni. Siku hizi za hatua zilisadifiana na Kongamano la Halmashauri ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hadhi ya Wanawake na kampeni zilizinduliwa katika Siku ya Kimataifa ya Wanawake Makundi ya haki za wanawake, vyama vya wafanyakazi na ya haki za ushuru yaliungana pamoja katika hatua za kampeni hizi katika zaidi ya mataifa 35.

Matakwa yaliyodaiwa kwa pamoja na makundi haya tofauti walituma ujumbe madhubuti wa pamoja yakitoa mwito kwa serikali kutimiza ahadi zao za kulinda haki za wanawake na usawa wa kiuchumi kwa kuchukua hatua za haki za ushuru. Kutokana na haya, serikali zilijitolea kufanya sera za ushuru kuwa za kiuendelevu ili kuunga mkono haki za wanawake na huduma za umma.  

Katika kujenga kampeni hizi, Kikao cha kwanza kabisa cha Haki za Ushuru kwa Haki za wanawake kilifanyika mnamo Juni jijini Bogota, nchini Colombia na azimio la kimataifa kuhusu haki za ushuru kwa wanawake likaandaliwa. Azimio hili lilitazamia kuwekea msingi matakwa ya pamoja ya kampeni kwa serikali na pia kujitolea upya kwa hitaji la haki za ushuru kwa haki za wanawake na kuwa matini ya marejeleo kuhusu ushuru na jinsia.

 

 

Share on Facebook Tweet this Email Print Share